Announcement

Maombi ya kazi za muda mfupi kwa ajili ya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam

University of Dar Es Salaam Computing Centre (UCC) ilishinda zabuni ya kuunda mfumo, kusambaza vifaa na kutoa huduma ya Uendeshaji wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam (DITF), maarufu kama Maoenesho ya Sabasaba yatakayoanza Juni 28 hadi Julai 13, 2021 kwenye viwanja vya Maonesho ya Sabasaba vilivyovyopo barabara ya Kilwa, Temeke -  Dar es Salaam.
Hivyo, UCC inapenda kutangaza nafasi za kazi za muda mfupi kwa ajili ya uendeshaji wa maonesho na kuuza Tiketi za watu na magari kuingia uwanjani.

SIFA ZA MWOMBAJI

 1. Awe mtanzania mwenye Umri usiozidi miaka thelathini (30);
 2. Awe na elimu ya kidato cha Sita au Diploma na kuendelea;
 3. Awe mwaminifu na mwenye uwezo wa kutunza fedha na vifaa vya kazi; na
 4. Awe na udhamini wa mfanyakazi wa University of Dar es salaam (UDSM)  au UCC.

MAOMBI YAAMBATANISHWE NA NYARAKA ZIFUATAZO:

 1. Barua ya Maombi ya Kazi
 2. Nakala ya Cheti cha Kidato cha Sita au Diploma
 3. Maelezo Binafsi (CV) yakionesha umri, anuani kamili, namba ya simu ya mkononi n.k.
 4. Picha ndogo (passport size)
 5. Taarifa za mdhamini wako kama vile jina kamili, idara anayofanyia kazi, na namba ya simu ya mkononi.
 6. Maombi yote yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wetu wa kielektroniki unaopatikana kupitia https://jobs.ucc.co.tz

Maombi yoyote yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au kuletwa moja kwa moja
Ofisini hayatafanyiwa kazi.


Mwisho wa kupokea maombi ni Juni 09, 2021

MUHIMU:

Unashauriwa kuweka jina lako kwenye majina ya nyaraka zako

mfano:

 • juma_manenge_photo.png, 
 • juma_manenge_f4.pdf,
 • juma_manenge_cert.pdf,
 • juma_manenge_f6.pdf,
 • juma_manenge_dip.pdf
 • juma_manenge_degree.pdf,
 • juma_manenge_letter.pdf,
 • juma_manenge_cv.pdf